• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wahimiza nchi wanachama zitekeleze makubaliano ya kutoa michango

    (GMT+08:00) 2017-06-28 09:56:49

    Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Bw Moussa Mahamat ametoa mwito kwa nchi wanachama zitekeleze makubaliano ya kutoa asilimia 0.2 ya makusanyo ya ushuru wa bidhaa za nje kwa ajili ya matumizi ya Umoja huo.

    Bw Mahamat amesema hayo alipohutubia ufunguzi wa mkutano wa 29 wa Umoja wa Afrika ulioanza jana huko Addis Ababa.

    Makubaliano hayo yaliyosainiwa na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika katika mkutano wa kilele wa 27 uliofanyika mwezi julai mwaka jana mjini Kigali, yalianza kutekelezwa mwezi Januari mwaka huu.

    Umoja wa Afrika umepanga kupata njia ya kuaminika ya kukusanya fedha kwa ajili ya amani barani humo kupitia mfuko wa amani wa Umoja huo, ili kupunguza utegemezi wa michango ya fedha kutoka kwa washirika wa nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako