• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Afrika Mashariki wahimizwa kuikwamua Burundi kutoka kwenye mvutano wa kisiasa

    (GMT+08:00) 2017-06-28 10:02:54

    Viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki EAC wamehimizwa kufanya mazungumzo na viongozi wa Burundi ili kuikwamua Burundi kutoka kwenye mvutano wa kisiasa.

    Mwenyekiti wa kituo cha utafiti na mpango wa mazungumzo Bw. Deo Hakizimana, amewataka viongozi wa kanda hiyo kushirikiana ili kukomesha mzozo wa kisiasa nchini Burundi kwa njia ya mazungumzo.

    Kwenye uzinduzi wa tuzo ya Macky Sall ya Mazungumzo barani Afrika (PMSDA) uliofanyika Nairobi, Bw. Hakizimana amesema jumuiya ya Afrika Mashariki ni jumuiya yenye nguvu, hivyo viongozi wa kanda hiyo wanatakiwa kujitokeza na kuihimiza serikali ya Burundi na wapinzani kuondoa hali ya kutoelewana ya muda mrefu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako