• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China apongeza ufunguzi wa baraza lisilo la kiserikali kuhusu hatua za kushirikiana na kuaminiana la Bara la Asia

    (GMT+08:00) 2017-06-28 17:37:24

    Mkutano wa pili wa baraza lisilo la kiserikali katika Mkutano wa utekelezaji wa hatua za kushirikiana na kuaminiana wa Asia umefunguliwa hii leo mjini Beijing.

    Akitoa salamu za pongezi katika mkutano huo, Rais Xi amesema mkutano huo umetoa njia muhimu kwa ajili ya kukuza mawasiliano na uaminifu na kuimarisha ushirikiano kati ya pande mbalimbali. Amesisitiza kuwa tangu China ilipokuwa mwenyeji wa mkutano huo mwezi Mei mwaka 2014, imekuwa ikifuata na kutekeleza mkakati wa usalama wa pamoja, jumuishi ushirikiano na endelevu barani Asia. Pia kuhimiza hatua ya kuanzisha mfumo mpya wa usalama na ushirikiano, kukuza ushirikiano wa hatua za uaminifu katika sekta mbalimbali, kuimarisha msingi wa sheria na ujenzi wa utaratibu katika mkutano huo, kupanua mtandao wa wenzi wa mkutano huo, na kuhimiza makundi ya umma kutoa mapendekezo yanayosaidia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako