• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan na Sudan Kusini zafikia makubaliano kuhusu kuongeza muda wa kufungua njia kupitisha msaada wa kibinadamu

    (GMT+08:00) 2017-06-28 18:14:44

    Vyombo vya habari vya Sudan Kusini vimeripoti kuwa, nchi hiyo na Sudan hivi karibuni zimefikia makubaliano kuhusu kuongeza muda wa kufungua njia ya kupitisha msaada wa kibinadamu.

    Kutokana na makubaliano hayo, mashirika husika yataweza kuendelea kuingia nchini Sudan Kusini kwa kupitia mpaka wa Sudan ili kutoa msaada wa kibinadamu kabla ya mwisho wa mwezi Juni mwaka ujao.

    Habari nyingine zinasema, naibu waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw. Abdul-Ghani Al-Naeem amesema kuondolewa kwa baadhi ya vikwazo kwa wakimbizi vilivyowekwa na rais Donald Trump wa Marekani hakutaathiri kuondoka vikwazo rasmi kwa Sudan mwezi Julai. Bw. Naeem amesema Sudan inaheshimu hatua ya Marekani ya kulinda usalama wa taifa, lakini serikali na watu wa Sudan sio tishio kwa usalama wa Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako