• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 795 wafariki kutokana na ugonjwa wa kipindupindu nchini Somalia tangu Januari

    (GMT+08:00) 2017-06-28 19:07:02

    Watu 795 wamefariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Somalia tangu Januari mwaka huu.

    Taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Ofisi ya uratibu wa masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA imesema, hadi kufikia mwezi huu, idadi ya wagonjwa wapya imepungua kwa asilimia 19, hali ambayo inachagiwa na juhudi zilizofanyika katika miezi kadhaa iliyopita.

    Asilimia 53 kati ya wagonjwa wote walioripotiwa ni watoto chini ya umri wa miaka mitano walioko Wadajir jimbo la Banadir, Harfo huko Mudug, Dusamareb iliyoko Galgadud na Markka katika jimbo la Lower Shebelle.

    Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watu milioni 5.5 wanakabiliwa na tishio la magonjwa yanayotokana na ukosefu wa maji safi ikiwemo kipindupindu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako