• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Miili 25 yapatikana katika ufukwe wa Tadjoura nchini Libya

    (GMT+08:00) 2017-06-28 19:15:27

    Chama cha Hilal Nyekundu cha Libya kimesema, wafanyakazi wake wamepata miili zaidi ya 25 katika ufukwe wa Tadjoura ulioko umbali wa kilomita 30 mashariki mwa Tripoli, mji mkuu wa Libya.

    Kwa mujibu wa chama hicho, huenda miili hiyo ni ya watu waliojaribu kuingia Ulaya kwa meli, lakini mpaka sasa chanzo cha vifo bado hakijajulikana.

    Wakati huohuo, kikosi cha ulinzi wa ufukwe cha Libya kimewaokoa wahamiaji 147 haramu waliojaribu kuingia barani Ulaya, wakiwemo wanawake 19 na watoto 4, ambao wengi wao wanatoka Cameroon, Sudan, Mali na Senegal.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako