• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Watumishi wa umma wenye mishahara ya chini wanapata ongezeko la asilimia 30

    (GMT+08:00) 2017-06-28 19:24:59

    Watumishi wa umma wanaofanya kazi kwa serikali kuanzia mwezi Julai tarehe 1 mshahara wao utaongezeka kwa kati ya asilimia 5.2 na asilimia 30.7.

    Watumishi wa umma wanaolipwa mshahara wa chini katika makundi ya kazi A hadi C na kundi la kazi D, watapata mshahara wa asilimia 17.46 na asilimia 27.02 na watapeleka nyumbani kati ya Sh12,192 na Sh14,442 kwa mtiririko huo.

    Wafanyakazi wanaoishi Nairobi katika makundi haya yakazi pia wataona posho yao ya nyumba ikipanda kutoka Sh3,000 hadi Sh3,750, hata posho kama misaada yao ya wageni bado haibadili Sh3,000.

    Wafanyakazi wa kikundi cha kazi N – ambao wanalindwa mkataba wa majadiliano ya pamoja (CBA) kati ya serikali na Umoja wa Watumishi wa Serikali ya Kenya (UKCS) mishahara yao imeongezeka kwa asilimia 6.84 na asilimia 24.34 Kwa jumla watapeleka nymbani Sh51,486 na Sh81,184 kwa mtiririko huo.

    Posho ya kila mwezi ya nyumba kwa wafanyikazi hawa, wanaoishi Nairobi katika makundi yao ya kazi imeongezeka hadi Sh35,000 kutoka Sh24,000, wakati marupurupu ya usafiri imeshuka hadi 6,000 kwa mwezi kutoka 8,000 na kwa mwezi.

    Malipo ya juu kwa watumishi wa umma ina maana serikali iko mbioni katika ukuaji wa kasi wa uchumi ili kusaidia matumizi yanayoongezeka.

    Ukuaji wa uchumi, hata hivyo, unatarajiwa kubaki nyuma kwa muda mfupi kutokana na madhara ya ukame, kupungua kwa mikopo ya sekta binafsi na kutokuwa na uhakika na uchanguzi mkuu ujao.

    Uchumi ulipanuka kwa asilimia 5.8 mwaka jana lakini, inatabiri kukua kwa asilimia 5.5 mwaka huu, kulingana na Benki ya Dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako