• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania Kampuni ya jasi kuwekeza bil. 30/-

    (GMT+08:00) 2017-06-28 19:26:51

    KAMPUNI ya utengenezaji wa jasi (gypsum) kutoka Ujerumani, KNAUF, imeingia rasmi katika biashara hiyo eneo la Afrika Mashariki na kuweka makao yake makuu nchini Tanzania, huku ikidhamiria kuwekeza kiasi cha dola milioni 15 (Sh bilioni 30) katika kipindi cha miaka michache ijayo.

    Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa KNAUF Afrika Mashariki, Zachopoulos Georgios, hadi sasa wameshawekeza kiasi cha dola milioni 10 (shilingi bilioni 21) na ni matarajio yao kwamba watafikisha bilioni 30 katika kipindi cha muda mfupi ujao.

    Kampuni hiyo ilianza rasmi shughuli zake nchini Tanzania, takribani miaka mitatu iliyopita na tayari imeajiri wafanyakazi 150; huku asilimia 99 kati yao wakiwa ni Watanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako