• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushiriki wa China barani Afrika ni mkubwa kuliko ilivyopendekezwa awali

    (GMT+08:00) 2017-06-29 09:19:56

    Ripoti iliyotolewa na shirika la ushauri la kimataifa la McKonsey imesema, ushiriki wa China barani Afrika ni mkubwa na wa pande nyingi kuliko tafiti za awali zilivyopendekeza.

    Ripoti hiyo imesema, mpaka sasa kuna kampuni zaidi ya elfu 10 za China zinazoendesha shughuli zao barani Afrika, ikiwa ni mara nne zaidi ya ilivyokadiriwa awali, na kati ya kampuni hizo, asilimia 90 ni za binafsi na zinahusika na sekta mbalimbali.

    Ripoti pia imesema uhusiano kati ya China na Afrika umeimarika katika mwongo uliopita, huku biashara kati ya pande hizo mbili ikikua kwa asilimia 20 kwa mwaka, na uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni ukikua kwa kasi zaidi na kufikia asilimia 40 kwa mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako