• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Europol latoa mapendekezo ya kuzuia mashambulizi mapya ya kirusi cha Kompyuta cha "WannaCry"

    (GMT+08:00) 2017-06-29 09:59:49

    Shirika la Polisi la Ulaya Europol jana limetoa mapendekezo ya kuzuia mashambulizi mapya la kirusi cha Kompyuta aina ya ransomware cha "WannaCry".

    Tovuti ya Shirika hilo imesema, kuna mapendekezo matano kwa ajili ya kuzuia kompyuta kuathiriwa na kirusi hicho, yakiwemo kutumia matoleo mapya ya programu na mifumo ya kompyuta, kuhifadhi data, kuweka programu za kompyuta za kujikinga dhidi ya virusi, kutotumia akaunti ya kompyuta yenye mamlaka ya msimamizi kwenye kazi za kawaida, na kutotembelea tovuti zinazotia mashaka.

    Kwa wahanga walioshambuliwa na kirusi hicho, Shirika hilo limependekeza kwamba wasilipe fidia, bali waite polisi na kufunga mtandao wa internet.

    Hivi sasa Europol limeunda timu ya dharura ya uratibu kwa ajili ya kudhibiti kuenea kwa kirusi hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako