• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raia 100 wauawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na muungano wa kimataifa mashariki mwa Syria

    (GMT+08:00) 2017-06-29 10:03:38

    Vyombo vya habari vya Syria na shirika la haki za binadamu nchini humo vimekadiria kuwa, mashambulizi ya anga yaliyofanywa na muungano wa kimataifa wa kupambana na kundi la Islamic State unaoongozwa na Marekani, yamesababisha vifo vya raia 100 mashariki mwa Syria, ambapo mashambulizi yaliyofanywa jana walisababisha vifo vya raia 40 katika mkoa wa Deir al-Zour, wengi kati yao wakiwa wanawake na watoto.

    Habari zinasema kuwa, jumanne wiki hii, kikosi cha muungano kilifanya mashambulizi dhidi ya mji wa Mayadeen, na kusababisha vifo vya raia wasiopungua 42, na jumatatu kikosi hicho kilishambulia gereza la kundi la Islamic State mjini humo, na kusababisha watu wasiopungua 57 kupoteza maisha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako