• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China awasili huko Hong Kong na kuhudhuria maadhimisho ya miaka 20 ya Hong Kong kurudi kwa China

    (GMT+08:00) 2017-06-29 16:17:06

    Rais Xi Jinping wa China amewasili Hong Kong kwa ziara ambako atahudhuria maadhimisho ya miaka 20 ya Hong Kong kurudi kwa China, na kuiapisha serikali ya awamu ya 5 ya mkoa wa utawala maalumu wa Hong Kong.

    Baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Hong Kong, rais Xi Jinping alitoa salamu kwa wakazi wa Hong Kong, na kusema anafurahi kufika tena Hong Kong baada ya miaka 9 iliyopita.

    Madhumuni yake ya ziara hiyo ni pamoja na kutoa pongezi kwa mafanikio yaliyopatikana Hong Kong katika miaka 20 iliyopita, kuonesha uungaji mkono wa serikali kuu ya China kwa uchumi wa Hong Kong, kuboresha maisha ya watu wa Hong Kong, na kupanga mustakabali wa Hong Kong ili kuhakikisha sera ya "nchi moja mifumo miwili" iendelee kwa utulivu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako