• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Washiriki wa Mkutano wa Baraza la Davos wajadili njia za kutimiza ongezeko shirikishi katika Mapinduzi ya nne ya viwanda

    (GMT+08:00) 2017-06-29 17:41:45

    Mkutano wa siku tatu wa mwaka wa awamu ya 11 ya Baraza la Davos wa majira ya joto umefungwa mjini Dalian, mkoani Liaoning, China. Wajumbe zaidi ya 2,000 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 90 duniani walijadili masuala yanayofuatiliwa duniani, ikiwa ni pamoja na changamoto zinazoukabili utandawazi duniani, kunufaika kwa pamoja ongezeko la uchumi na matumizi ya teknolojia mpya. Kauli mbiu ya mkutano huo ilikuwa "kutimiza ongezeko shirikishi katika Mapinduzi ya nne ya viwanda".
    Kauli ya "Ongezeko shirikishi" ilitolewa kwa mara ya kwanza mwaka 2007 na Benki ya Maendeleo ya Asia, na inaonekana mara kwa mara katika sera na mawazo ya maendeleo yanayotekelezwa na serikali ya China, na kukubaliwa na nchi nyingi duniani. Mwenyekiti wa bodi ya Kundi la Lang Chao linaloongoza makundi mengine katika sekta ya Cloud Computing Bw. Sun Pishu anaona kuwa, ongezeko shirikishi linazingatia fursa zenye usawa, linafaidika na ongezeko la uchumi kwa njia yenye usawa na mwafaka, na kuhimiza jamii na uchumi kupata maendeleo yenye uwiano na endelevu. Kwa maoni ya Bw. Sun Pishu, uchumi wa dijitali ni ufunguo wa kutimiza ongezeko hilo. Anasema: "Ili kutimiza ongezeko shirikishi, inapaswa kuanzisha mazingira yenye kiini cha dijitali na jukwaa la dijitali inayohusisha habari mbalimbali, ambapo watu wote wanaweza kutumia kwa usawa. Kwa upande mwingine, viwanda vinatakiwa kuongeza kiwango cha matengenezo yasiyochafua mazingira na kutumia uwezo wa kiakili katika matumizi ya pamoja ya kidijitali. Hizo ni pande mbili muhimu za ongezeko shirikishi." Naibu mkurugenzi wa utendaji wa Mfuko unaotoa msaada kwa watu maskini Bw. Wang Xi ameeleza kuwa, ongezeko shirikishi linamaanisha kuwa, wakati linapokuza uchumi chini ya mazingira ya uchumi wa soko, linatakiwa kuzingatia suala la usawa, na kuhakikisha maslahi ya watu wenye hali duni. Bw. Wang Xing anasema: "Kwa maoni yangu, lengo la ongezeko shirikishi ni kuhakikisha suala la usawa wakati linapotimiza ongezeko la uchumi. Kwa watu wa kawaida, wale waliotajirika mapema wanatakiwa kuwasaidia wale walioko nyuma kiuchumi. Wakati huo huo, serikali inatakiwa kutunga sera zinazosaidia maendeleo ya watu maskini, hususan sera za kuwainua watu maskini kote nchini. Naona kuwa China imepata mafanikio mazuri katika sekta hiyo." Katika hotuba aliyotoa wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa baraza la Davos la Majira ya Joto, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ameeleza kuwa, ajira ni msingi wa kuhakikisha ongezeko shirikishi, ambalo halitatimizwa bila ya kuwa na nafasi za kutosha za ajira. Mwenyekiti wa bodi ya kampuni binafsi ya gesi ya Asia Kusini ya India ( South Asia Gas Enterprise PVT. LTD) Bw. Subodh Kumar Jain amesema kuwa, ongezeko shirikishi vilevile ni changamoto kubwa inayoyakabili maendeleo ya India kwa hivi sasa, na njia muhimu ya kutatua suala hilo ni kuongeza nafasi za ajira. Anasema: "Naona kuwa ongezeko shirikishi litatimizwa wakati tunapozingatia namna ya kuongeza nafasi za ajira katika miji midogo na sehemu za vijijini."
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako