• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya biashara ya China yasema tuhuma za Umoja wa Ulaya kuwa China ni kiini cha bidhaa feki si za kuwajibika

    (GMT+08:00) 2017-06-29 18:13:48

    Wizara ya biashara ya China imesema ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na Umoja wa Ulaya inayosema kuwa China ni mzalishaji mkubwa duniani wa bidhaa feki si ya kuwajibika.

    Ripoti yenye kurasa 74 iliyotolewa na idara ya ujasusi wa mali ya Umoja wa Ulaya inasema mwaka 2015, China bara na Hong Kong zilijihusisha na asilimia 86 ya bidhaa feki duniani zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 396.5. Msemaji wa Wizara ya biashara ya China Bw Sun Jiwen amesema uhalisi na ukweli kuhusu ripoti hiyo vinatakiwa kuchunguzwa.

    Mwaka 2015 China ilianzisha kampeni kubwa ya kusimamia ubora wa bidhaa zake zinazouzwa nje, na miezi minne ya kwanza ya mwaka huu imeshughulikia kesi zaidi ya 4,600 zinazohusu bidhaa zinazosafirishwa nje.

    Bw Sun amesema serikali ya China itaendelea kuchukua hatua kupambana na bidhaa feki hasa kwa zile zinazosafirishwa kwenda nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako