• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kenya imeagiza tani 35,000 za mahindi kutoka Uganda kwa mwezi mmoja

    (GMT+08:00) 2017-06-29 19:20:30

    Kenya imeagiza tani 35,000 za mahindi kutoka nchi jirani ya Uganda ndani ya mwezi mmoja uliopita za thamani ya dola milioni $20.6.

    Hata hivyo Kenya bado inahitaji mahindi zaidi kwani matumizi ya kila mwezi ni tani elfu 27,000.

    Mwezi uliopita aidha Kenya iliagizia mahindi ya tani 30,000 kutoka Mexico ili kupunguza bei ya unga iliokuwa imefikia dola 1.8.

    Waziri wa kilimo Willy Bett anasema serikali imeanzisha njia kadhaa za kusambaza mahindi ili kufika maeneo yote ya nchi.

    Amesema baadaye mwezi Juni meli nyingine yenye tani 74,646 za mahindi inatarajiwa katika bandari ya Mombasa.

    Uzalishaji wa mahindi katika eneo la bonde la ufa nchini Kenya ulipungua kutoka tani milioni 1.89 hadi tani milioni 1.4 kutokana na kupungua kwa mvua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako