• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: EABL kufungua kiwanda kipya Kisumu

    (GMT+08:00) 2017-06-29 19:20:55

    Kampuni ya kuzalisha mvinyo nchini Kenya East African Breweries inapanga kufungua kiwanda kipya mjini Kisumu kwa gharama ya shilingi bilioni 15.

    Kiwanda hicho kimesaidi kandarasi na wakulima 45,000 ambao watakuza mawele ya kuzalisha bia.

    Miongoni mwa wakulima waliosaini kandarasi na kampuni hiyo ni pamoja na wale wa kaunti za Siaya, Migori, Kisumu, Homa Bay, Kitui, Makueni na Tharaka Nithi ili kukithi mahitaji ya kampuni hiyo ya tani 20,000 za nafaka kila mwaka.

    Rais Uhuru Kenyatta amesema jana kwamba kiwanda hicho kitasaidia kuongeza mahitaji ya mawele nchini hadi tani 40,000 kwa mwaka.

    Uzinduzi wa ujenzi wa kiwanda hicho unatarajiwa Julai 16 na oparesheni kuanza ndani ya miaka 2.

    Kiwanda hicho kitaajiri kwa njia mbali mbali zaidi ya watu 110,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako