• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Rwanda yasaini makubaliano ya dola milioni 500 na benki ya Afreximbank

    (GMT+08:00) 2017-06-29 19:21:40

    Rwanda na benki ya Afreximbank zimesaini makubaliano ambapo benki hiyo itaipa Rwanda dola milioni $500 za miradi ya maendeleo ya kibiashara.

    Benki hiyo ambayo inafanya mkutano wake mkuu wa mwaka inajadili na serikali kuhusu maeneo ya maendeleo ya kibiashara zitakapoelekezwa fedha hizo.

    Rais wa benki hiyo Dkt. Benedict Oramah, amesema wanatarajia kufadhili miradi kadhaa ya kusukuma mbele biashara za kitaifa.

    Baadhi ya maeneo inakofikiria serikali ni kama vile viwanda, kupanua shirika la ndege la RwandAir na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Bugesera.

    Naye waziri w fedha na mipango ya kiuchumi Claver Gatete amesema serikali inashirikiana kwa karibu na benki hiyo ili kukuza miradi ya kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako