Wachimba madini wadogo wadogo katika eneo la Mubende nchini Uganda wamemuomba rais Yoweri Museveni kuwasaidia ili wasifurushwe kutoka eneo lao la kuchimba.
Maelfu ya wachimbaji wako kwenye eneo la kilomita tano mraba lakini wanahofia watafurushwa ili eneo hilo litumike kuchimba dhahabu na kampuni kubwa.
Mwenyekiti wao John Bosco Bukya, amesema ikiwa wataondolewa basi zaidi ya watu 25,000 watakosa ajira,
Tarehe 13 mwezi huu agizo la kuwafurusha wachimbaji hao lilitolewa baada ya mkutano kati ya Rais Museveni na wasimamizi wa kampuni ya
Gemstone International lakini sasa wanasema rais hakushauriwa vizuri kuhusu hatua ya kutaka kuwafurusha.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |