• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Wafanyabiashara Kampala wataka bunge kuwapa sheria mpya ya ulipaji wa kodi

    (GMT+08:00) 2017-06-29 19:22:28

    Wafanyabiashara mjini Kampala nchini Uganda wametoa makataa ya siku 9 kwa spika wa bunge nchini humo Rebecca Kadaga kuwapa sheria mpya kuhusu ulipaji wa kodi ya nyumba za kibiashara.

    Chini ya chama chao cha Kacita wafanya biashara hao wamesema wanampa spika hadi tarehe 6 Julai ili kutoa tarehe kamili ya kuwa na sheria kuhusu mahusiano ya wenye nyumba na wapangaji.

    Msemaji wa Kacita Issa Sekito mesema ni makosa kwa serikali kutrgemea sheria ya ulipaji kodi ya mwaka 1949.

    Amesema wapangaji mara nyingi wanasumbuliwa na wenye nyumba kwa kufurushwa bila notisi na pia kwa kukosa kandarasi za upangaji ili hali wenye nyumba ndio wanafaa kuzitoa.

    Aidha wafanyabiashara hao wanataka kuwepo na uthibiti kuhusu uuzaji wa jumla na wa reja reja wa umeme kwani kuna watu wanatumia ulaghai kujinufaisha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako