• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Serikali yasema viwanda vingi mikoa ya Pwani sio nia mbaya.

    (GMT+08:00) 2017-06-29 19:23:23

    Serikali ya Tanzania imesema uwepo wa viwanda vingi mikoa ya Pwani hauna nia mbaya.

    Hayo yamesemwa leo (Alhamisi) na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isaac Kamwelwe alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Kisangi aliyetaka kufahamu Serikali imejipanga vipi kukabili madhara yatokanayo na viwanda vya saruji vilivyopo mikoa ya Dar Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na Tanga.

    Alisema uamuzi wa wapi kiwanda kijengwe hutegemea soko la bidhaa, upatikanaji wa malighafi na teknolojia.

    Maeneo ya ukanda wa Pwani kutoka Tanga mpaka Mtwara amesema yana faida ya upatikanaji wa malighafi na gharama nafuu za usafirishaji kwa zinazoagizwa kutoka nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako