• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi wa Kenya wawaokoa watoto wawili baada ya shambulizi la kigaidi

    (GMT+08:00) 2017-06-29 19:34:25

    Maofisa wa usalama wa Kenya wamethibitisha kuwa wamewaokoa watoto wawili kati ya watoto wanne wa shule ambao hawajulikani walipo kufuatia shambulizi linaloshtakiwa kufanywa na kundi la Al-Shabaab huko Lamu.

    Kamishna wa kaunti ya Lamu Bw. Joseph Kanyiri amesema, watoto hao wameokolewa katika operesheni iliyofanywa huko Boni.

    Pia amesema watoto hao wamejeruhiwa miguuni na vichwani na sasa wamepelekwa hospitali mjini Nairobi kwa ajili ya matibabu.

    Imefahamika kuwa watu zaidi ya nane wakiwemo watoto wanne na polisi wanne wameuawa katika shambulizi linaloaminika kufanywa na wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako