• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ni rasmi sasa fainali ni Chile dhidi ya Ujerumani kombe la Mabara

    (GMT+08:00) 2017-06-30 08:58:05

    Baada ya timu ya taifa ya Chile kutangulia fainali ya Kombe la mabara hapo juzi, jana mabingwa wa dunia Ujerumani walikuwa wakipepetana na Mexico kutafuta mshindi mwingine wa kwenda katika fainali.

    Mchezo huo ulionekana mapema sana kwamba unaweza kuwa wa upande mmoja tofauti na wa juzi kwani kipindi cha kwanza tu tayari Ujerumani walitangulia kifua mbele kwa mabao mawili kwa sifuri.

    Alikuwa Leon Goretzka akitumia dakika 2 kufunga mabao mawili, alianza dakika ya 6 na wakati Mexico wanaendelea kushangaa akawafunga la pili dakika ya 8 kabla ya kipindi cha pili Timo Werner kuifungia Ujerumani bao la 3.

    Wakati watu wakiamini huenda mchezo huo ukaisha kwa matokeo ya 3 kwa 0, Marco Fabian aliifungia Mexico na kufanya kuwa 3-1 kabla ya Amin Younes kuipatia bao la mwisho Ujerumani na matokeo kuisha kwa mabao 4 kwa 1.

    Matokeo hayo yanawafanya mabingwa hao wa dunia timu ya taifa ya Ujerumani kukutana na mabingwa wa America Chile katika mchezo mgumu sana ambao utapigwa siku ya Jumapili kuamua nani bingwa wa Kombe la mabara mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako