• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taifa Stars yasonga hatua ya robo fainali michuano ya COSAFA

    (GMT+08:00) 2017-06-30 08:58:27

    Timu ya Taifa la Tanzania, Taifa Stars ambayo ipo kwenye michuano ya COSAFA 2017 inayoendelea Afrika Kusini, jana ilirudi uwanjani kucheza mchezo wa mwisho wa Kundi A dhidi ya Mauritius huku Malawi wakicheza dhidi ya Angola.

    Katika Kundi A timu zote nne zilikuwa na nafasi ya kufuzu hatua inayofuata kabla ya michezo ya jana ambapo Tanzania na Angola zilihitaji ushindi au sare ya magoli ili mmoja kati yao afuzu, Malawi na Mauritius kila mmoja alikuwa anahitaji ushindi.

    Taifa Stars imefanikiwa kufuzu hatua ya robo-fainali baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Mauritius ikiwa ni dakika moja baada ya Mauritius kupata goli la kuongoza dakika ya 67, Simon Msuva aliisawazishia Taifa Stars dakika ya 68.

    Mchezo wa Malawi na Mauritius nao ulimalizika kwa sare ya 0-0 na kutokana na matokeo hayo Tanzania imesonga mbele na itacheza na Afrika Kusini baada ya kuongoza kwa tofauti ya magoli licha ya kuwa na point 5 sawa na Angola. Malawi na Mauritius zimemaliza zikiwa na point 2 kila moja katika hatua hiyo ya makundi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako