• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mabingwa wa Ligi Kuu ya Raga ya Kenya, KCB waweka kambi Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2017-06-30 08:59:21
    Mabingwa mara tano wa Ligi Kuu ya Raga ya Kenya, KCB, wamefunga safari kuelekea Afrika Kusini ili kujinoa kwa msimu wa 2017/2018 utakaoanza baadaye mwaka 2017. Kikosi hicho cha wachezaji 29 na maafisa watano wa benchi la kiufundi kiliwasili jana katika uwanja wa ndege wa Tambo jijini Johannesburg saa moja usiku kabla ya kuelekea mjini Cape Town ambako kinakita kambi yake. Baadhi ya wachezaji waliopo safarini ni Peter Waitere (nahodha), Shaban Ahmed, Nick Ongeri, James Kilonzo, Marlin Mukolwe, Rocky Aguko na Joshua Macharia.

    Afisa kutoka Benki ya KCB, James Asiko Owiro alisema safari ya Afrika Kusini ni muhimu sana katika maandalizi ya klabu ya KCB hasa chipukizi wake.

    Mbali na Ligi Kuu ya Kenya, KCB pia walishinda taji la Enterprise Cup kwa mara ya tatu mfululizo na sita kwa jumla mwaka 2017.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako