• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Usajili: tetesi za usajili wa soka kwa siku ya Alhamis barani Ulaya

    (GMT+08:00) 2017-06-30 08:59:50

    Baadhi ya tetesi za usajili barani ulaya zilizotufikia ni kwamba Mshambuliaji wa Watford Stefano Okaka, 27, amepewa dau kubwa la kuhamia Shanghai Shenhua ya hapa China. Naye Pierre Emerick-Aubameyang, 28, anayenyatiwa na Liverpool anaonekana kukaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda Tianjin Quanjian ya hapa China, ambayo imetoa dau la pauni milioni 70

    Chelsea nao huenda wakavuruga dau la Zenith St Petersburg la pauni milioni 26 la kumtaka beki wa Roma, Kostas Minolas, huku mchezaji huyo pia akisita kuhamia Urusi. Na beki wa Chelsea Nathan Ake, 22, anakaribia kufanikisha uhamisho wake wa pauni milioni 20 kwenda Bournmouth.

    Michel Keane hatarajiwi kurejea Burnley kwa sababu Everton wanatarajiwa 'kulazimisha' usajili wake kabla ya kumalizika kwa wiki hii. Michael Keane atagharimu pauni milioni 25. Naye winga wa timu hiyo Gerard Deulofeu, 23, amekataa nafasi ya kurejea Barcelona, huku AC Milan na Juventus pia zikimtaka

    Arsenal wameambiwa lazima walipe pauni milioni 57 ili kumsajili Alexandre Lacazette, 26, kutoka Lyon. Naye kinda wa Arsenal Kaylen Hinds anajiandaa kuondoka Emirates na kujiunga na Wolfsburg ya Ujerumani. Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale yuko tayari kuondoka Hispania na kuhamia Manchester United.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako