• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa TFF kutotetea tena kiti chake, asweka rumande hadi Julai 3

    (GMT+08:00) 2017-06-30 09:00:28

    Rais wa Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ambaye anakabiliwa na tuhuma za utakatishaji fedha na kughushi nyaraka za Shirikisho hilo ili ajipatie fedha huenda asionekane tena kwenye kinyang'anyiro cha kugombea Urais kwani tayari ameswekwa rumande mpaka Julai 3 mwaka huu.

    Malinzi hataweza kutetea kiti chake kwani zoezi la usaili kwa wanaogombea nafasi mbalimbali za uongozi (TFF) limeanza jana na litamalizika Jumamosi ya tarehe 1 Julai. Malinzi amefikishwa jana mahakamani akiwa na katibu wake, Mwesigwa Celestine wakikabiliwa na mashitaka 28, katika kesi hiyo Jamal Malinzi anakabiliwa na mashitaka zaidi ya 25 mengi yakiwa ni ya kughushi nyaraka zaidi ya 20 za malipo katika michakato ya malipo mbalimbali .

    Shitaka lingine ni la utakatishaji fedha kiasi cha zaidi ya dola laki 3 za kimarekani na hii ni kwa wote watatu, Malinzi, Mwesigwa na Afisa wa fedha wa TFF, Nsiande Mwanga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako