• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zatakiwa kutumia teknolojia na nishati endelevu kupunguza madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2017-06-30 09:20:04

    Serikali za nchi za Afrika zimetakiwa kufanya ubunifu na kuchanganya teknolojia za kisasa za gharama nafuu, pamoja na matumizi ya nishati endelevu kupunguza madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa.

    Mtaalamu wa shirika la maendeleo la Umoja wa mataifa UNDP Bw Biplove Chaudhary amewaambia wataalamu wanaohudhuria mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na usalama wa chakula mjini Juba, Sudan Kusini, kuwa serikali za Afrika zinatakiwa kufuata kanuni za kilimo cha kisasa na usimamizi mzuri wa maliasili, ili kupunguza madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa. Amesema pamoja na kuwa nchi za Afrika hazichangii sana kwenye mabadiliko ya hali ya hewa, sekta ya kilimo barani Afrika ndiyo yenye hatari zaidi ya kuathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Mtaalamu wa Shirika la mpango wa mazingira la Umoja wa mataifa UNEP Bw David Smith amesema utulivu wa kisasa unategemea matumizi endelevu ya maliasili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako