• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Somalia yataka kuwaunganisha wasomali wanaorudi na wenyeji

    (GMT+08:00) 2017-06-30 09:20:25

    Serikali ya Somalia imefungua mkutano wa siku mbili wenye lengo la kuweka uhusiano wa karibu kati ya wasomali wanaorudi kutoka nje na wale waliokuwepo nchini Somalia.

    Mkutano huo unahudhuriwa na maofisa wa serikali kuu na za majimbo, wanataaluma, wasomali wenyeji na wale wanaorudi kutoka nje, ili kutafuta amani na masikilizano na kusaidia kutuliza nchi.

    Kwenye ufunguzi wa mkutano huo Bw Mohamed Abdi Abdilahi, Waziri wa HirShabelle anayeshughulika mipango, ushirikiano wa kimataifa na uhusiano wa diaspora, aliwataka wasomali wanaorudi na wenyeji kuondoka tofauti zao na kuleta utulivu wa nchi.

    Rais Mohamed Abdulahi Farmajo aliahidi kuwa atafanya juhudi ya kuwaunganisha wasomali.

    Wenyeji nchini Somalia wamekuwa wakilalamika kuwa kazi zote nzuri nchini Somalia zinachukuliwa na wasomali wanaorudi kutoka nje, wakati waliokuwepo nchini Somalia wakiachwa kuhangaika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako