• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Iraq latwaa msikiti wa Al-Nuri mjini Mosul

    (GMT+08:00) 2017-06-30 09:44:35

    Jeshi la Iraq limetangaza kuwa limetwaa tena udhibiti wa eneo la msikiti wa Al-Nuri mijini Mosul.

    Msemaji wa kituo cha uongozi wa operesheni za pamoja za jeshi la Iraq amesema kikosi cha kupambana na ugaidi kimewafurusha wapiganaji wa Kundi la IS kutoka kwenye eneo la msikiti wa Al-Nuri, katikati ya mji mkongwe wa Mosul.

    Waziri mkuu wa Iraq Bw Haider al-Abadi ametoa taarifa akitaja kukombolewa kwa msikiti wa Al-Nuri kama ishara ya kulitokomeza kundi la "Islamic State", na kusema jeshi la serikali litaendelea kuwasaka magaidi hadi wote watakapoangamizwa.

    Wizara ya ulinzi wa Marekani imesema jeshi la Iraq kinatarajiwa kuudhibiti tena mji wa Mosul baada ya muda mfupi. Msemaji wa wizara hiyo Bw Ryann Dillon amekadiri kuwa mji wa Mosul utakombolewa na jeshi la Iraq baada ya siku chache, lakini Kundi la IS litaendelea kuwepo kwenye sehemu mbalimbali nchini Iraq.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako