• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi 24 wa Afrika watarajiwa kuhudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika Ethiopia

    (GMT+08:00) 2017-06-30 09:45:23

    Viongozi 24 wa nchi za Afrika wanatarajiwa kushiriki kwenye mkutano wa kilele wa 29 wa Umoja wa Afrika utakaofanyika tarehe 3 na 4 mwezi Julai mjini Addis Ababa, Ethiopia.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia Bw Meles Alem amesema rais Mahmoud Abbas wa Palestina pia anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo.

    Kwa mujibu wa Wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia, viongozi wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na rais Ellen Johnson wa Liberia, rais Muhammadu Buhari wa Nigeria, rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria na Mfalme Mswati III wa Swaziland.

    Mkutano huo utajadili masuala ya amani na usalama barani Afrika, maandalizi ya kuanzisha Eneo la Biashara Huria la Afrika CFTA na utekelezaji wa Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako