• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zatazamiwa kutimiza maendeleo ya kasi kupitia ushirikiano na China

    (GMT+08:00) 2017-06-30 09:53:41

    Mchumi mkuu wa zamani wa Benki ya Dunia na profesa wa Chuo Kikuu cha Beijing Bw. Lin Yifu amesema nchi za Afrika zinatarajiwa kutimiza maendeleo ya kasi kutokana na ushirikiano na China.

    Bw. Lin Yifu alisema hayo jana alipohojiwa wakati wa kuhudhuria mkutano wa mwaka wa Benki ya EXIM ya Afrika huko Kigali, Rwanda. Amesema nchi za Afrika zikiboresha miundombinu na kuendeleza viwanda vinavyohitaji nguvu kazi nyingi kupitia ushirikiano na China, ikiwemo mradi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", pia zinaweza kupata maendeleo ya kasi kama nchi za Asia ya Mashariki zilivyojiendeleza baada ya vita kuu ya pili ya dunia.

    Amesema ushirikiano kati ya China na Afrika umepata mafanikio hatua kwa hatua. Ametolea mfano wa reli za Addis Ababa-Djibouti na Mombasa-Nairobi zilizojengwa na makampuni ya China, zilizohimiza maendelea ya mawasiliano ya reli katika nchi za Afrika, na kiwanda cha vitatu nchini Ethiopia kilichowekezwa na kampuni ya Huajian ya China na kuleta faida nyingi za kiuchumi na kijamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako