• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China kufanya ziara Russia na Ujerumani, na kuhudhuria mkutano wa G20

    (GMT+08:00) 2017-06-30 09:56:49

    Wizara ya mambo ya nje ya China imetoa taarifa kuwa rais Xi Jinping wa China atafanya ziara nchini Russia na Ujerumani, na kuhudhuria mkutano wa kilele wa 12 wa kundi la nchi 20 kuanzia tarehe 3 hadi tarehe 8 Julai.

    Msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Li Huilai amesema, nchini Russia rais Xi Jinping atakutana na rais Vladmir Putin na kuhakikisha mwelekeo na lengo la maendeleo ya uhusiano kati ya China na Russia, kuzidisha uaminifu wa kisiasa na kimkakati, kusukuma mbele ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Chao amesema, huu ni mwaka wa 45 tangu China na Ujerumani zianzishe uhusiano wa kibalozi, ziara ya rais Xi Jinping nchini humo itahakikisha lengo jipya la maendeleo kati ya pande mbili na kutilia nguvu mpya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ulaya.

    Rais Xi Jinping pia anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa kilele wa 12 wa kundi la nchi 20 utakaofanyika tarehe 7 hadi tarehe 8 Julai mjini Hamburg, Ujerumani na kueleza maoni ya China kuhusu hali ya uchumi wa dunia na ushirikiano wa kiuchumi wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako