• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa laongeza muda wa kikosi cha ulinzi wa amani huko Darfur

    (GMT+08:00) 2017-06-30 16:25:26

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuongeza muda wa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur kwa mwaka mmoja, hadi tarehe 30 mwezi Juni mwaka ujao.

    Katika azimio hilo lililopitishwa jana, Baraza hilo limesema hali ya usalama huko Darfur bado si nzuri, na mgogoro kati ya makabila ni sababu kuu ya matumizi ya mabavu katika eneo hilo.

    Idadi ya watu waliokimbia makazi yao huko Darfur imeongezeka kufikia milioni 2.7 na watu milioni 2.1 wanahitaji msaada wa binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako