• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sekta ya uzalishaji nchini China zaongezeka kwa miezi 11 mfululizo

  (GMT+08:00) 2017-06-30 16:25:48

  Sekta ya uzalishaji nchini China imeendelea kuongezeka kwa miezi 11 mfululizo, ikiashiria nguvu ya nchi hiyo ambayo ni ya pili kwa ukubwa wa uchumi duniani.

  Takwimu zilizotolewa na Idara ya Takwimu ya China zimeonyesha kuwa, kiashiria cha kusimamia uzalishaji nchini China kilifikia 51.7 mwezi huu, ikiwa ni ongezeko kutoka 51.2 mwezi uliopita.

  Wakati hali inaonekana kuwa nzuri, baadhi ya viwanda vya jadi ikiwemo viwanda vya kutengeneza mafuta, makaa ya mawe, na bidhaa zisizo za madini ya chuma bado zinakabiliwa na shinikizo la kushuka kwa uzalishaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako