• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema hakuna anayeweza nia thabiti ya serikali na watu wa China ya kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi

    (GMT+08:00) 2017-06-30 17:35:24

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lu Kang amesema, hakuna mtu anayeweza kubadilisha nia thabiti ya serikali na watu wa China ya kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi.

    Lu Kang ametoa kauli hiyo kufuatia uamuzi wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani wa kutangaza kuiuzia Taiwan zana za kijeshi zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.4. Bw. Lu amesema, China imetoa malalamiko makali kwa Marekani ikipinga kithabiti uamuzi huo, pia inaihimiza Marekani kufuata ahadi ilizotoa katika taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani na kuondoa mipango ya kuiuzia silaha Taiwan. Pia amesema China inaitaka Marekani kusimamisha uhusiano wa kijeshi kati yake na Taiwan, ili kuepusha kuharibu zaidi uhusiano kati ya China na Marekani na ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta muhimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako