• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kituo cha Polisi chashambuliwa huko Kinshasa, DRC

    (GMT+08:00) 2017-06-30 18:18:14

    Mapigano makali yametokea kati ya polisi na watu walioshambulia kituo cha polisi huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, na kusababisha vifo na majeruhi ya watu kadhaa huku baadhi ya wafungwa wakitoroka.

    Wizara ya mambo ya ndani ya DRC imetoa taarifa ikisema, shambulizi hilo limefanywa na kundi la watu wasiojulikana.

    Msemaji wa polisi nchini humo amesema, hivi sasa hali imedhibitiwa, na kwamba mshambuliaji mmoja aliuawa kwenye mapigano na wengine watatu wamekamatwa, huku askari wanne wakijeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako