• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuendelea kushiriki kwenye mchakato wa utekelezaji wa makubaliano ya pande zote kuhusu suala la nyuklia la Iran

    (GMT+08:00) 2017-06-30 18:18:56

    Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema, China itaendelea kushiriki kwenye mchakato wa utekelezaji wa makubaliano ya pande zote kuhusu suala la nyuklia la Iran na kuhimiza maendeleo ya utekelezaji wa makubaliano hayo kwa manufaa ya pande mbalimbali, ili kutoa mchango katika kutatua suala la nyuklia la Iran.

    Bw. Wu amesema hayo katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la nyuklia la Iran. Amesema, katika mwaka mmoja uliopita tangu makubaliano hayo ya pande zote kuanza kutekelezwa, hali ya ujumla ya utekelezaji wa makubaliano hayo ni imara, na umuhimu ni kuendelea kusukuma mbele utekelezaji wa makubaliano hayo.

    Pia amesema, China inapongeza Iran kutekeleza ahadi husika kufuata matakwa ya makubaliano ya pande zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako