Waziri wa Kilimo wa Afrika Kusini Bw. Senzeni Zokwana amesema, nchi hiyo imeamua kusimamisha mauzo ya kuku hai baada ya kutokea mlipuko wa homa ya mafua ya ndege katika mashamba mawili yaliyoko mkoani Mpumalanga nchini humo.
Bw. Zokwana amesema, hatua hiyo imeleta wasiwasi tangu baadhi ya mifugo kuathiriwa na ugonjwa huo, lakini hatua hiyo imechukuliwa kutokana na maslahi ya taifa na wafanyabiashara wengi wa kuku.
Afrika Kusini imeripoti mgonjwa wa pili wa homa ya mafua ya ndege huko Standerton mkoani Mpumalanga, baada ya mlipuko wa kwanza kutokea karibu na Villiers jumanne iliyopita katika eneo hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |