• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Kenya breweries kufungua kiwanda kipya

    (GMT+08:00) 2017-06-30 19:07:02

    Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kwamba kampuni ya East Africa Breweries itafungua kiwanda kipya cha kutengeneza pombe mjini Kisumu, mradi ambao utabuni nafasi elfu-110 za ajira.

    Rais Kenyatta alisema kiwanda hicho kipya cha pombe kinachojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni-15 kitasaidia wakulima elfu-30 katika kaunti za Kisumu, Siaya, Homa-Bay, Migori, Tharaka Nithi, Machakos na Makueni kupata kandarasi za kukuza mtama kwa niaba ya kampuni ya East Africa Breweries.

    Amesema mahitaji ya mtama yameongezeka sambamba na idadi ya wakulima wanaopewa kandarasi ya kukuza zao hilo.

    Rais alisema kilimo kitakuwa na manufaa ikiwa wakenya watabadili mbinu za ukulima na kukuza mazao ya kuwapa tija badala ya mimea ya chakula.

    Tangu mwaka wa 2013, zaidi ya kampuni-1,500 zimewekeza hapa nchini huku zaidi ya kampuni-20 za kimataifa zikichagua Kenya kuwa kitovu cha shughuli zao barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako