• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi: Sera ya "Nchi Moja na Mifumo Miwili" itekelezwe kikamilifu

    (GMT+08:00) 2017-07-01 10:35:50

    Rais Xi Jinping amesema serikali kuu ya China itaendelea kufuata kithabiti sera ya "Nchi Moja na Mifumo Miwili", na kuhakikisha kuwa sera hiyo inatekelezwa kikamlifu katika mkoa wa utawala maalumu wa Hong Kong.

    Amesisitiza kuwa, kufuata na kutekeleza kanuni za "Nchi Moja Mifumo Miwili" kunalingana na maslahi ya watu wa Hong Kong na kusaidia kudumisha ustawi na utulivu huko Hong Kong, pia ni maslahi ya kimsingi ya taifa na matakwa ya pamoja ya watu wote wa China.

    Rais Xi ametoa kauli hiyo akihutubia maadhimisho ya miaka 20 ya Hong Kong kurudi kwa China iliyofanyika leo asubuhi huko Hong Kong, ambapo baraza la serikali ya awamu ya 5 ya mkoa wa utawala maalumu wa Hong Kong pia limeapishwa.

    Vile vile rais Xi Jiping ameitaka Hong Kong itoe kipaumbele kufanikisha maendeleo, ambayo amesema ni jambo muhimu la kwanza kwa Hong Kon, pia ni ufumbuzi wa maswala mbalimbali yanayoikabili Hong Kong.

    Amesisitiza kuwa, China Bara imepata maendeleo ya kasi kwa mfululizo katika miaka ya karibuni, hali ambayo inatoa fursa nzuri kwa Hong Kong. Ni muhimu kwa Hong Kong kuchukua fursa hizo katika juhudi zake za kupata maendeleo zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako