• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Burundi aitisha michango ya kifedha kwa uchaguzi wa 2020.

    (GMT+08:00) 2017-07-01 16:52:55

    Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza siku ya Ijumaa amewahimiza wananchi watoe michango ya kifedha kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2020 nchini humo. Nkurunziza amesema kuwa kwa kuzingatia hali ambazo Burundi ilipitia tangu mwaka wa 1961, inahitaji kujiandaa vizuri uchaguzi huo na uchaguzi mwingine ujao bila kuomba msaada wa kifedha kutoka kwa washirika wa kimataifa.

    Amesema kuwa akaunti imefunguliwa katika Benki Kuu ya Burundi ambapo wafadhili wanaweza kutoa michango ya kifedha kwa uchaguzi mkuu wa nchi. Na kuzitaka benki na taasisi zingine za kifedha kushirikiana na benki kuu kuwezesha mpango huo kwa wale ambao wanataka kutuma michango yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako