• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mgogoro wa kijeshi uliotokea kusini mashariki mwa jamhuri ya Afrika ya Kati wasababisha vifo vya watu 22

    (GMT+08:00) 2017-07-01 17:36:45

    Vyombo vya habari vya jamhuri ya Afrika ya Kati Ijumaa vilitoa habari kuwa mgogoro wa kijeshi uliotokea hivi karibuni huko Zemio, mji wa kusini mashariki mwa nchi hiyo umesababisha vifo vya watu wasiopungua 22.

    Habari zinasema kuwa, kuanzia tarehe 28 mwezi Juni, wakazi wa Zemio na wanamgambo wa huko walipambana kutokana na mabishano ya mali. Pande hizo mbili hazikukubali hukumu ya mahakama, na mabishano yalizidi kuwa mapambano ya kijeshi. Wanamgambo kutoka Bangassou pia walijiunga na mapambano hayo. Hivi sasa ujumbe wa kulinda utulivu wa Umoja wa Mataifa nchini jamhuri ya Afrika ya Kati umeongeza kupeleka askari wa kulinda amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako