• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanamgambo 13 wanaounga mkono serikali ya kijeshi wauawa na kundi la Taliban kaskazini mwa Afghanistan.

    (GMT+08:00) 2017-07-02 18:13:24

    Wanamgambo 13 wanaounga mkono serikali waliuawa kufuatia shambulio la Taliban lililotokea mapema leo katika jimbo la Balkh kaskazini mwa Afghanistan.

    Msemaji wa serikali ya jimbo Farhad Munir ameliambia shirika la habari la China, Xinhua kuwa, wapiganaji wa Taliban walivamia msikiti mmoja uitwao Masjed-e-Safad uliopo kwenye kijiji cha wilaya ya Chimtal na kuua wanamgambo 13 wa kikabila.

    Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo wamesema, washambuliaji hao walikuwa wamevaa sare za kijeshi na msikiti pia uliharibiwa baada ya kushambiliwa kwa risasi.

    Wapiganaji wa Taliban wamesema wanahusika na shambulizi hilo. Waliwahimiza raia kukaa mbali na mikusanyiko rasmi, misafara ya kijeshi na vituo vilivyodhaniwa kama malengo yao, pia waliwaonya watu wasiunga mkono serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako