• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 8 wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa kufuatia milipuko ya magari mji mkuu wa Syria, Damascus

    (GMT+08:00) 2017-07-02 18:13:39

    Watu wapatao wanane wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa kwenye milipuko ya mabomu yaliyotegwa kwenye magari matatu huko Damascus, mji mkuu wa Syria asubuhi ya leo.

    Wakazi wa mji wa Damascus waliamka baada ya kushtushwa na sauti ya milipuko mitatu, ambayo baadaye ilijulikana imesababishwa na magari matatu ya kujitoa muhanga.

    Mamlaka ya mji huo iliyatilia shaka magari hayo, kabla ya magari mawili kulipuka karibu na barabara ya uwanja wa ndege kwenye mlango wa kuingia mji wa Damascus kabla ya kufikia malengo yao ndani ya jiji, huku gari la tatu lilikimbilia mnara wa Tahriri mashariki ya Damascus.

    Habari zinasema, magaidi walikuwa na lengo la kulipua magari hayo kwenye maeneo ya mkusanyiko wa watu katika mji mkuu huo, ambako watu wamerejea kazini baada ya kusheherekea sikukuu ya Eid-el Fitr.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako