• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Qatar yakataa matakwa 13 yaliyotolewa na nchi zilizositisha uhusiano wa kibalozi

    (GMT+08:00) 2017-07-02 19:16:17

    Waziri wa mambo ya nje wa Qatar ambaye yuko ziarani nchini Italia Bw. Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani amesema Qatar inakataa matakwa yaliyotolewa na nchi zilizositisha uhusiano wa kibalozi na nchi yake, kwa sababu matakwa hayo yamekwenda kinyume na sheria za kimataifa, yanalenga kuidhuru mamlaka ya Qatar badala ya kupambana na ugaidi.

    Hivi karibuni nchi nne ikiwemo Saudi Arabia ilitoa matakwa 13 kwa Qatar yakiwa ni sharti la kutatua suala la kusitisha uhusiano wa kibalozi, na kuilazimisha Qatar kutimiza matakwa hayo ndani ya siku 10 kabla ya tarehe 2 Julai. Matakwa hayo ni pamoja na Qatar kurudisha wanadiplomasia wote nchini Iran, kusimamisha ushirikiano wa kijeshi na Iran, kufunga kituo cha televisheni cha Aljazeera, na kusimamisha ujenzi wa kituo cha jeshi la Uturuki nchini Qatar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako