• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wataka uwekezaji zaidi kwa vijana ili kuchochea maendeleo

    (GMT+08:00) 2017-07-03 08:37:52

    Umoja wa Afrika umetoa wito kwa nchi wanachama wake kuimarisha uwekezaji wao kwa vijana ikiwa ni sehemu muhimu ya kujenga bara lenye maendeleo.

    Kamishna wa rasilimali watu, sayansi na teknolojia wa Umnoja wa Afrika Bw. Martia De-Paul Ikounga amesema elimu na kuwawezesha vijana ni mambo muhimu katika ajenda ya kisiasa ya Umoja wa Afrika. Amesema elimu, kuendeleza ujuzi, na ujasiriamali vinapaswa kuwa malengo makuu ya nchi wanachama wa Umoja huo katika nia ya bara hilo ya kuleta maendeleo endelevu na amani ya kudumu.

    Wakati huohuo, naibu mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Thomas Kwesi Quartey amesema, Afrika, ambayo inawajibika kwa asilimia 4 za utoaji wa hewa chafu duniani, ndio inaathirika zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa. Bw. Quartey amezitaka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kufanya kazi zaidi katika kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa kutekeleza hatua madhubuti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako