• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini akataa kukutana na timu ya majadiliano nchini Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2017-07-03 08:38:08

    Kiongozi wa kundi kuu la waasi la Sudan Kusini SPLA-IO anayeishi uhamishoni Riek Machar amekataa kukutana na ujumbe wa maofisa wa mjadala wa kitaifa wa Sudan Kusini.

    Msemaji wa kundi hilo Lam Paul Gabriel amesema, kiongozi huyo ambaye kwa sasa anazuiliwa nyumbani nchini Afrika Kusini, amekataa kukutana na timu hiyo kwa sababu mjadala wa kitaifa sio muhimu kama kusimamisha vita nchini Sudan Kusini. Amesema kundi hilo halitashiriki kwenye mjadala huo isipokuwa kama amani itapatikana kwanza.

    Jopo la ngazi ya juu la maofisa wa Sudan Kusini likiongozwa na mwenyekiti mwenza wa Tume ya Mjadala wa Kitaifa lilikwenda nchini Afrika Kusini ili kumshawishi Riek Machar kujiunga na mjadala huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako