• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya auhakikishia Umoja wa Ulaya kuwa uchaguzi mkuu utafanyika kwa amani

    (GMT+08:00) 2017-07-03 09:26:28

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya jana aliuhakikishia Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya EOM kuwa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi ujao utakuwa wa amani.

    Akizungumza na waangalizi hao jijini Nairobi hapo jana, Rais Kenyatta amesema Kenya itafanya uchaguzi mkuu wa kuaminika, wenye uhuru na haki, na kwamba serikali yake imechukua hatua za kuhakikisha haki ya kidemokrasia ya wananchi wake ya kuwachagua viongozi wao bila ya kuingiliwa.

    Ameongeza kwamba serikali yake pia itahakikisha Kenya inakuwa na usalama na amani katika kipindi cha uchaguzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako