• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakutaja Marekani kupeleka tena manowari katika bahari ya visiwa vya Xisha vya China kuwa uchokozi wa kisiasa na kijeshi

    (GMT+08:00) 2017-07-03 09:50:26

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amekitaja kitendo cha Marekani kutuma tena manowari zake katika bahari ya visiwa vya Xisha vya China kama "uchokozi mkubwa wa kisiasa na kijeshi", na kusema serikali ya China inapinga kithabiti kitendo hicho.

    Bw. Lu amesema, Manowari ya Stethem ya Marekani jana iliingia katika bahari ya visiwa vya Xisha vya China, baadaye China ikapeleka manowari na ndege za kivita kuonya na kuifukuza manowari hiyo kwenye eneo hilo.

    Pia amesema, hivi sasa chini ya juhudi za China na nchi za Asia Kusini Mashariki, hali ya Bahari ya Kusini inaendelea kutulia na kuonesha mwelekeo mzuri. Amesisitiza kuwa China inaitaka Marekani isimamishe mara moja vitendo vya uchokozi vitakavyoharibu mamlaka ya China na kutishia usalama wa China.

    Amesisitiza kuwa China itaendelea kuchukua hatua zote za lazima kulinda mamlaka na usalama wa taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako