• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya maendeleo ya BRICS yasema theluthi mbili ya miradi itakuwa ya ujenzi wa miundombinu endelevu katika miaka mitano ijayo

    (GMT+08:00) 2017-07-03 09:51:00

    Benki ya maendeleo ya nchi za BRICS imetangaza mkakati wa jumla wa miaka mitano ijayo, ambapo Benki hiyo itaweka kipaumbele katika maendeleo endelevu, na theluthi mbili ya mikopo itatumiwa kusaidia ujenzi wa miundombinu endelevu.

    Kwa mujibu wa mkakati huo, Benki hiyo itaweka kipaumbele katika nishati safi, umwagiliaji na ulinzi wa vyanzo vya maji safi.

    Katika siku za baadaye, Benki hiyo inapanga kuanzisha shughuli katika nchi zisizo za BRICS, huku ikianza maandalizi ya masharti, utaratibu na matakwa ya kusajili nchi wanachama wapya. Ushiriki wa nchi wanachama wapya utaisaidia benki hiyo kuinua ushawishi wa kimataifa na kuongeza akiba ya mitaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako